Kuhusu Msimbazi Senta
Msimbazi Senta, ni kituo kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Kituo kilianza tangu mwezi Machi mwaka 1961 kikiwa na lengo la kuondoa umasikini kupitia huduma mbalimbali za kijamii.
Kituo cha Msimbazi kinasimamiwa na Mkurugenzi Padre Audax Kaasa akisaidiwa na Mhasibu na Meneja. Kituo kina endeshwa na bodi ya Wakurugenzi ambayo ipo chini ya
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mhashamu Jude Thaddeaus Ruwaichi.
Mkurugenzi wa Kituo cha Msimbazi Padre Audax Kaasa
Meneja wa Kituo cha Msimbazi, Joseph Ntilema
Asili ya kituo hiki inafuatiliwa kutoka mwanzoni mwa miaka ya 1960, ambapo kilianza kama kituo cha elimu ya watu wazima na kuanza kutumika rasmi mnamo Juni,
1962, ambapo kilizinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa zamani na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa. Ukweli huu unasaidiwa sana na jiwe la uzinduzi ambalo linapatikana
mbele ya Ukumbi wa Maranta, katika kituo cha Msimbazi. Habari hii ya maandishi inasema: "Jumba hili la maendeleo lilitolewa na Wafanyakazi Katoliki
wa Uswizi kama alama ya umoja na mapendo, likafunguliwa na Waziri Mkuu Mh. Bwana Rashidi Kawawa mbele ya Ujumbe wa Ndugu
hao wa Uswizi, Mheshimiwa, Bwana, Augustine Steffen 17/06/1962."