Semina za Ndoa
Kwa zaidi ya miaka hamsini, kituo cha Msimbazi kimekuwa na jukumu kubwa la kutoa semina kwa wanandoa watarajiwa. Semina hizi zimekuwa zikiwahusisha wakufunzi wa ndoa wenye uzoefu wa muda mrefu katika ndoa zao. Pia kituo kimekuwa kikitoa ushauri nasaha kwa wanandoa wenye changamoto mbalimbali katika ndoa zao. Kwa kipindi kirefu semina hizi za ndoa zimekuwa zikiratibiwa na Padre Novatus Mbaula.Mratibu wa Ndoa Jimbo Padre Novatus Mbaula akitoa mafundisho kwa Wanandoa watarajiwa katika ukumbi wa Jubilei Msimbazi Senta
Wanandoa watarajiwa wakisikiliza mafundisho ya ndoa katika ukumbi wa Jubilei, Msimbazi Senta
Wanandoa watarajiwa wakisikiliza mafundisho kutoka kwa Mratibu wa Ndoa Jimbo Padre Novatus Mbaula